M-KOBA, Vodacom

M-KOBA ni nini?

M-KOBA ni huduma ya kifedha inayoendeshwa na Vodacom kwa ushirikiano na TPB Bank inayolenga kuwezesha wateja wa M-Pesa kufungua na kuendesha Akaunti za kuweka akiba kwa makundi huku wakifurahia huduma za kifedha. Bidhaa hii itazingatia kutoa mazingira mazuri kwa vikundi vya kuchanga fedha kama VICOBA, VSLA na vile vya kifamila na marafiki kufanya kazi kwa muda halisi ili kuhakikisha wanapunguza gharama za uendeshaji, usalama na uwazi kati ya wanachama na kikundi kwa ujumla. Hii inamaanisha wale wenye vikindi vya kuchanga fedha wataweza kujiandikisha wenyewe kupitia M-KOBA na kuendesha vikundi vyao kwa njia ya kidigitali. Huduma hii itapatikana kupitia M-Pesa. Wateja watapiga *150*00# kisha bonyeza Huduma ya Fedha kisha kuchagua M-KOBA.

Kuna Akaunti ngapi kwenye bidhaa ya M-KOBA?

A: M-KOBA inajumuisha Akaunti mbili mbazo mteja ataweza kutumia:

  • Marafiki/Familia
  • VICOBA/VSLA

Marafiki/Familia 
Hii ni akaunti maususi kwa vikundi vidogo inaweza kuwa familia ama marafiki ambao wamekusudia kuchanga fedha na baadae kugawana baada ya muda Fulani. Mfano: UPATU.

VICOBA/VSLA 
Hii ni akaunti maususi kwa ajili ya vikundi vyenye upana mkubwa wa wanachama na vilivyo na mfumo wa kuuza na kununua hisa, kuweka akiba, Michango ya Kijamii na Kupeana Mikopo. Vikundi hivi ni vile vihusishavyo VICOBA/VSLA/CB/SILC

Nani anaweza kufungua Akaunti ya M-KOBA?

Wateja wa Vodacom wanaotumia M-Pesa pekee ndio watakaoweza kufungua Akaunti ya M-KOBA.

Vigezo vya kufungua akaunti ya M-KOBA ni vipi?

1.Kikundi cha M-KOBA kitatakiwa kuwa na wanachama wasiopungua wanne.

2. Ili kutengeneza akaunti ya M-KOBA Kila kikundi kinapaswa kuwa na viongozi watatu. 
Mwenyekiti 

Katibu 
Mwekahazina

Je kuna ada yoyote mteja anayolipia kutumia M-KOBA

Hakuna ada wala makato yoyote kwa mteja atakapo fungua au kutumia Akaunti ya M-KOBA. Kutakuwa na gharama ndogo ya tozo ya Tsh.100 pale mteja takapokuwa akiangalia salio la Michango.

Je, kuna ada yoyote ya mteja atakayolipa wakati wa kutuma pesa kutoka M-Pesa kwenda kwenye akaunti ya M-KOBA?

Hakuna ada yoyote mteja atakayolipa kwa kutoa pesa kwenye Akaunti yake ya M-Pesa kwenda kwenye akaunti ya Kikundi au kutoa pesa kwenye akaunti ya kikundi kwenda kwa mwanakikundi.

Je ni taarifa gani ambazo Vodacom itazitoa kwa benki ya TPB pindi nitakapo fungua au kujiunga na Akaunti ya vikundi ya M-KOBA?

Mteja atakapo kuwa akifungua au kujiunga na Akaunti ya M-KOBA taarifa za kawaida za Mteja zitatumwa kutoka Vodacom kwenda kwenye benki ya TPB. Taarifa hizi ni Jina la Mteja, Namba ya simu, Jinsia na Umri wa mteja. Hivyo kabla ya kufungua au kujiunga na Akaunti ya M-KOBA mteja atatakiwa kukubali vigezo na Masharti.

Viongozi wa Vikundi ndo nani?

Kila kikundi kwenye M-KOBA kitakuwa na viongozi watatu ambao ni: 
MWENYEKITI: Yeye ndiye mwanzilishi na msimamizi wa kikundi. Ana mamlaka ya kuongeza mwanachama yeyote na kuchagua viongozi wengine na yeye ndiye mtu wa mwisho kuidhinisha uhamisho wa malipo kwa mwanachama yeyote 
KATIBU: Anaongezwa na mwenyekiti wa kikundi na ndiye anayeanzisha malipo yote na Mkopo kwa wanachama wengine.
MWEKAHAZINA: Anaongezwa na mwenyekiti wa kikundi, ana mamlaka ya kuthibitisha Malipo na Mikopo inayotolewa kwa wanachama.

Je, tunahamishaje fedha kutoka kwa akaunti ya kikundi cha M-KOBA kwenda kwenye Akaunti ya mtu ya M-Pesa?

Fedha zitahamishwa kupitia awamu tatu, Katibu ataanzisha mchakato wa malipo kutoka kwa akaunti ya kikundi kwa mwanachama kisha Mwekezaji atahakiki Malipo na Mwenyekiti wa kikundi ataidhinisha Malipo ndopo fedha zitahamishwa kutoka kwa Akaunti ya Kundi kwenda kwa mwanachama alie kusudiwa.

Ninawasiliana nani nikiwa na malalamiko, maswali, mapendekezo au ombi?

Wateja watatakiwa kuwasiliana na Huduma kwa wateja ikiwa wanamalalamiko au Mapendekezo juu ya bidhaa ya M-KOBA. Wataje watatakiwa kupiga 100.

Ni nini kinachofanyika wakati wa mgogoro wa kundi?

Ikiwa itatokea mgogoro kwa wanachama wa kikundi kutokana na kutoelewana juu ya fedha za kikundi wanakikundi watahitajika kuripoti polisi. Baada ya kuripoti polisi watapewa kibali Maalumu na kuwasilisha Vodacom ili kuzuia fedha za kikundi kutoka. baada ya kupokea ruhusa ya Polisi Vodacom itazuia fedha za akaunti ya kikundi na wanachama wa kikundi watahitajika kutatua tena tofauti zao polisi na kupata kibali kingine cha kuruhusu Vodacom kufungua fedha zao za kikundi.

PAKUA KIJITABU KWA KUGUSA LINK HAPA CHINI

https://drive.google.com/file/d/0B7KOdQNugdNQVlBKVmg2ZHc3ODdzQWhSR0JuejV2RU5FUnow/view?usp=sharing

7 Comments to “M-KOBA, Vodacom”

  1. Ombeni Munuo

    Je mtu anaweza pata mkopo akiwa nyumbani kwakutulia simbila kwenda benk
    Na je wanakikundi watakuwa wanakusanyaje hisa zao kama nikwanjia ya. M-pesa je ikitokea mwanakikundi hajawatuma hisa yake atawajibishwa vip?

    Reply

Post Comment